Rio Olympic: Fursa kwa Vijana, Watembea Wakiuza Kondom Mitaani
Rio, Brazil
WANAMICHEZO wengi walioko Rio
nchini Brazil kwa ajili ya michuano ya 2016 Rio Olympics wameonekana
kufanya vitu tofauti sana mwaka huu ili kuwawezesha kila mmoja kupata
kile anachokidhamiria kwenye mashindano hayo. Kila mmoja yuko ‘bize’
kujituma ili ahakikishe angalau anapata medali kama ilivyo kawaida kwa
tuzo za mashindano hayo.
Matukio mengi yameripotiwa kutokea huko
Rio, lakini kuna hili la njemba mmoja aliyejulikana kwa jina la Eric,
yeye na vijana wenzake wamekuwa wakitembea na mifuko ya kondomu mitaani
huku wakihamasisha ngono salama kwa wanamichezo hao.
Wamekuwa wakionekana kwenye maeneo
tofauti katika Jiji la Rio huku wakiuza kondomu hizo tena hadharani kama
machinga anavyotembeza vyombo na nguo mtaani tena bila aibu. Hii
imeonekana kuwa fursa kwa vijana hao kwenye mashindano kwa kuwa kuna
wageni wengi ambao wanatumia zana hiyo.
Baada ya kuhojiwa na wanahabari wa E!
News, Eric amejibu haya; “Mimi sioni aibu kuuza kondomu hadharani kwa
maana ni biashara inayoniingizia kipato…. kuna baadhi ya wanamichezo
hawafanyi kabisa ngono wakiwa kwenye mashindano makubwa kama haya,
lakini kuna wengine wanaamini bila kufanya ngono hawawezi kufanya vizuri
kwenye michezo yao na kupata tuzo, hao ndiyo wateja wangu haswa, ”
alisema Eric.
Post a Comment