EXCLUSIVE: NEEMA YANGA, FIFA YAFUNGUA DIRISHA LA USAJILI, NI KWA SAA 48 TU
Kuna taarifa kwamba Shirikisho la Soka la Kimataifa limefungua tena dirisha la usajili kwa saa 48.
Taarifa
kutoka ndani ya TFF zinasema Kuanzia leo, dirisha hilo la usajili
litafungwa Jumapili saa 6 usiku, kwenda Jumatatu na hii ni nafasi kwa
klabu ambazo hazikuwasilisha usajili kukamilisha.
Mabingwa
wa Tanzania, Yanga pamoja na Coastal Union pia African Lyon zilikuwa
kati ya timu za Ligi Kuu Bara na Daraja la Kwanza ambazo hazikuwa
zimekamilisha usajili.
Hii
inaweza kuwa nafasi ya klabu hizo kumalizana na suala hilo ili kutulia
na kulenga maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza Ligi Kuu Bara, wiki
ijayo.
Post a Comment