Ndege yaanguka mtini, yateketea na kuua sita

Virginia, Marekani
Ndege ndogo iliyokuwa na watu sita imeanguka kwenye mti na kuteketea kwa moto wakati ikijaribu ikitua Uwanja wa Ndege wa Shannon Kaskazini mwa Jimbo la Virginia nchini Marekani, watu wote sita waliokuwemo kwenye ndege hiyo wameripotiwa kufariki dunia jana Ijumaa.
Mashuhuda wa tukio hilo waliokuwa wakisafii kwa treni wamesema walianza kuona moshi na baadaye moto ukiwaka na waliposogea eneo la tukio waliona ndege ndogo ikiwa imeanguka juu ya mti huku ikiteketea kwa moto. Aidha tarifa zimeeleza pia kuwa hakuna mtu aliyeokolewa hata mmoja, wote waliokuwemo wamefariki dunia.
Polisi katika Jimbo la Virginia wamesema watu wote waliokufa siyo raia wa Marekani na kwamba miili ya marehemu hao itapelekwa kwa Daktari Mkuu wa jimbo hilo, Richmond kwa uchunguzi ili kuwatambua na kubaini ndugu zao.
SOURCE: DAILY MAIL

No comments

Powered by Blogger.