UMEIPATA HII YA MAKONDA, WALIMU KUSAFIRI BURE KWENYE TRENI DAR?


Dar es Salaam,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewatangazia walimu wa mkoa huo, kuanza kusafiri bure kwenye treni baada ya kuingia makubaliano na Shirika la Reli Tanzania (TRL).
Hatua hiyo imekuja ikiwa miezi michache imepita tangu, kiongozi huyo kuanzisha mfumo wa walimu kusafiri bure kwenye daladala wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Makonda alisema walimu watasafiri bure katika njia za Stesheni-Ubungo Maziwa na Stesheni –Pugu ambako treni zinafanya safari zake.
“Kinachotakiwa ni kuwa na vitambulisho kutoka kwa wakuu wa shule, wakionyesha hakuna atakayewahoji hivyo watasafiri bure,”alisema Makonda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa alisema walimu watasafirishwa kwa nidhamu kubwa.

No comments

Powered by Blogger.