OFFICIAL: MGOSI ASTAAFU RASMI SOKA, SASA KUWA MENEJA WA SIMBA SC


                                                               Musa hassan “mgosi”.
 MSHAMBULIAJI mkongwe na nahodha wa Simba SC, Mussa Hassan Mgosi amestaafu rasmi soka na sasa anakuwa Meneja wa timu hiyo. Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Manara amethibitisha hilo na kusema Mgosi ataagwa rasmi katika mchezo wa kirafiki kwa kimataifa utakaopigwa Jumapili ya juma hili uwanja wa Taifa Dar es Salaam dhidi ya URA ya Uganda.
Manara ameeleza kwamba aliyekuwa Meneja wa timu, Abbas Suleiman Ally anakuwa Mratibu wa timu (Team Coordinator) kuanzia leo na nahodha mpya ni Jonas Mkude.
Aidha, kiungo wa klabu hiyo,  Peter Mwalyanzi aliyesajiliwa msimu uliopita akitokea timu ya Mbeya City FC, ametolewa kwa mkopo African Lyon iliyopanda kucheza ligi Kuu msimu huu wa 2015/2016.
Simba wataingia kwenye mechi na URA wakiwapa nafasi mashabiki wao kukiona kikosi chao kwa mara ya pili uwanja wa Taifa baada ya Agosti 8 mwaka huu siku ya Simba Day kuichapa 4-0 AFC Leopard ya Kenya.Inaelezwa mechi na URA itakuwa ya mwisho  ambapo Agosti 20 wataanza ligi kuu kwa kuchuana na Ndanda FC uwanja wa Taifa.

No comments

Powered by Blogger.