Dirisha la Usajili Ulaya Limefungwa Usiku wa Leo na Hawa.
Vilabu
vya soka barani ulaya vimefanya usajili wa kumarisha vikosi vyao katika
siku ya mwisho ya usajili uliofungwa usiku wa kuamkia Septemba mosi.
Chelsea wamemrejesha beki wao kisiki
David Luiz waliomuuza miaka miwili iliyopita kwa Paris St- Germain,
mchezaji huyu kanunuliwa kwa kiasi cha pauni million 34. Pia Chelsea
imemsajili Marcos Alonso toka Fiorentina kwa pauni milion 23.
Moussa Sissoko amesajiliwa na Tottenham
akitokea Newcastle kwa pauni milioni 30, Leicester City wamesajili Islam
Slimani toka Sporting Lisbon kwa pauni 29.
Stoke City wamemsajili Wilfried Bony kwa
mkopo toka Manchester City, Samir Nasri nae amepelekwa kwa mkopo
Sevilla toka kwa matajiri wa Man City
Mshambuliaji Mario Balotelli wa
Liverpool amesajiliwa na Nice ya Ufaransa bure, West Ham wamsajili beki
Alvaro Arbeloa toka Real Madrid,
Valencia ya Hispania wamesamjili kwa
mkopo wa muda mrefu Eliaquim Mangala wa Manchester City, Nao Juventus
wamemsajili Juan Cuadrado kwa mkopo toka Chelsea kwa mkataba wa miaka
mitatu.
Jack Wilshere ametua Bournemouth kwa
mkopo wa msimu mzima, Mshambuliaji Mkongo Dieumerci Mbokani asajiliwa na
Hull City. Enner Valencia aenda Everton kwa mkopo hadi mwisho wa msimu
kutoka West Ham.
Post a Comment