Hatimaye Aliyekuwa Rais wa Brazil Aenguliwa Rasmi Madarakani
Aliyekuwa Rais wa Brazil, Dilma Rousseff.
Makamu wa rais , Michel Temer ambaye amemrithi Bi Rousseff kwa muda, amekula kiapo cha urais hadi ifikapo January 2019.
Rais
Mpya wa Brazil, Michel Temer amesema nchi yake inaingia katika enzi
mpya ya matumaini baada ya kuondoshwa madarakani kwa aliyekuwa rais wa
nchi hiyo Dilma Rousseff.
Akizungumza na taifa hilo kupitia
Televisheni, Rais Temer ametoa wito wa kuungana pamoja na kusema kuwa
kuondolewa madarakani kwa Bi. Rousseff kumemaliza miezi kadhaa ya
mashaka.
Rais Mpya wa Brazil, Michel Temer.
Wabunge nchini humo walipiga kura ya
kutokuwa na imani na Bi. Rousseff ya kumuondoa madarakani kwa asilimia
61 huku kura 20, zikipinga kuondolewa kwake.
Amekutwa na hatia ya udanganyifu wa bajeti ya nchi hiyo wakati wa kampeni zake za uchaguzi miaka miwili iliyopita.
Makamu wa rais , Michel Temer ambaye amemrithi Bi Rousseff kwa muda, amekula kiapo cha urais hadi ifikapo January 2019.
Katika majibu yake ya kwanza ya kura
zilizopigwa, Bi Rousseff amesema kuwa, Baraza la Seneti halikutenda haki
kwa mwanamke asiye na hatia.
Aidha amewashutumu Maseneta ambao walipiga kura ya kumuondoa madarakani kwamba wamehusika katika mapinduzi ya kisiasa.
Post a Comment