BEACH BOY WANAVYOBAKA MABINTI COCO BEACH JIJINI DAR
. Mwanamme anayejiita Beach Boy akiendelea kumfundisha dada mmoja kuogelea.
Beach Boy akiwa kamkumbatia dada huyo
Baadhi ya mabinti na wanawake wengine wanaofika kwenye Ufukwe wa Coco uliopo Oysterbay jijini Dar kwa lengo la kufundishwa kuogelea, wamekuwa wakijikuta wanafanyiwa vitendo vichafu, ikiwemo kubakwa na wanaume wanaojiita Beach Boys, Risasi Mchanganyiko lina mkanda kamili.
INAKUAJE?
Akisimulia mchezo mzima unavyokuwa, kijana mmoja ambaye ni mwenyeji wa maeneo hayo alisema: Watu wanapokwenda beach, wasichana wengi wanapenda kuogelea na wengi wao hawajui, hivyo wale Beach Boys wanaokodisha maboya huingia nao kwenye maji kwa lengo la kuwafundisha. Kinachofuata sasa, Beach Boys hupeleka boya hadi kwenye kina kirefu, wakifika huko kijana huomba apewe penzi huku akimtishia mdada kuwa akigoma anamuachia afe. Mdada akijifanya mbishi anazamishwa, anakunwya maji kidogo kisha anaibuliwa, akishaona mlango wa kuzimu anakubali kiulainii. Kwa staili hii wadada wengi wamepewa mimba na kuambukizwa magonjwa
MSIKIE MHANGA
Mmoja wa mabinti aliyewahi kufanyiwa mchezo huo aliyeomba hifadhi ya jina lake alidai kuwa, kuna wakati alifika na wenzake kwa lengo la kufundishwa kuogelea lakini kilichompata hatasahau. Mimi kila wakati nikienda kule beach natamani sana kuogelea lakini nilikuwa siwezi ndo nikaambiwa wale vijana wanaokodisha yale maboya ukitaka wanakufundisha. Siku moja nikaenda pale, nikaongea na kijana mmoja ambaye alikubali kunifundisha kwa malipo ya shilingi elfu tano. Wakati ananifundisha akawa ananipeleka kwenye sehemu yenye maji mengi, tukaenda mbali sana ambako nisingeweza kurudi peke yangu. Huko akaanza kunitaka nimpe penzi huku akisema hata nisipomlipa, kwa kweli nilichangayikiwa. Wakati najifikiria alishaanza kunichezea kisha akanibaka, alidai binti huyo.
OFM KAZINI
Baada ya kupata madai hayo, makamanda wa OFM wikiendi iliyopita walitinga katika eneo hilo na kukuta vijana wakiendelea na zoezi la kuwafundisha kuogelea watu mbalimbali, asilimia kubwa wakiwa ni wanawake. Katika uchunguzi uliofanyika ilibainika kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa vitendo vya ubakaji kuchukua nafasi kwenye zoezi hilo kutokana na mazingira yalivyo. Akizungumzia tuhuma hiyo, mmoja wa ma-beach boys aliyejitambulisha kwa jina la Faridi alisema: Unajua tunaofanya kazi hii tuko wengi na kila mmoja ana tabia zake, hivyo siwezi kukataa kuwa vitendo hivyo havipo. Ila wakati mwingine hawa tunaowafundisha wanatupa mtihani kwa mavazi yao na viuchokozi vyao, sasa sisi kama wanaume tuliokamilika wakati mwingine inakuwa ngumu kuvumilia, alisema kijana huyo.
POLISI WAWAFUNGIA KAZI
Kufuatia vitendo vya ubakaji kushamiri maeneo hayo, jeshi la polisi hivi karibuni lilifanya doria na kuwakamata watu 33 wakiwemo Beach Boys huku Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro akisema kuwa watuhumiwa hao wamenaswa baada ya askari kufanya msako na kukutwa wakifanya mapenzi kwenye Ufukwe wa Bahari ya Hindi.
TAHADHARI
Gazeti hili linapenda kuwatahadharisha wazazi na mabinti zao kuwa makini na vijana hao ambao wameonekana kuwa tatizo. Epuka kufundishwa kuogelea na mtu ambaye humjui na wala huna imani naye. CHANZO: GAZETI LA RISASI JUMATANO

Post a Comment