MAUA : BILA YA MWANA FA NISINGEKUWA HAPA


Maua Saleh Sama.


JUNI 13, mwaka jana kulikuwa na tukio kubwa la utoaji tuzo kwa wasanii wa muziki nchini zilizojulikana kama Kili 2015 ambazo zilifanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar.
Katika tuzo hizo kulikuwa na msanii mmoja wa kike ambaye alikuwa akiandika historia kwa mara ya kwanza ya kuibuka kidedea katika tuzo hizo katika kipengele cha Wimbo Bora wa Reggae/Dance Hall (Wimbo Let Them Know).

Msanii huyo alikuwa ni Maua Saleh Sama ambaye aliibukia katika Wimbo wa So Crazy akimshirikisha MwanaFA.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Maua alitinga ndani ya Mjengo wa Global Publishers ulioko Bamaga-Mwenge jijini Dar ambapo moja kwa moja aliwekwa katika Kipindi cha Mtu Kati kinachorushwa na Global TV Online.
Katika makala haya yanaeleza alichofunguka;

Kwa nini kazi zako ziNAchalewa sana kutoka?
“Ujue mwanzoni nilikuwa chuoni (Chuo Cha Ushirika na Biashara, Moshi) na kipindi hicho nilikuwa nikifanya muziki huku nasoma kwa hiyo nikawa nashindwa kujigawa sawa, ila kwa sasa nipo freshi ukiangalia hata wimbo wangu wa sasa wa Mahaba Niue haujapishana sana na wa Let Them Know.”
Ulikutana vipi na Mwana FA?   


(Anacheka kidogo...)  “Well, MwanaFA ni mmoja kati ya wanamuziki niliokuwa nawakubali sana na nilikuwa pia na ndoto ya kufanya nao muziki siku moja. Basi kuna wimbo wangu wa So Crazy niliuimba (demo) lakini nikashangaa rafiki yangu mmoja kamtumia MwanaFA bila ya mimi kujua na baada ya siku kadhaa FA akanipigia simu.

“Akaniambia kuwa amesikiliza wimbo wangu, ameupenda sana kwani nina sauti nzuri ya kuimba hivyo atakuwa tayari kunisimamia katika kazi zangu na pia kuimba naye, nikamkubalia na hapo ndipo ukawa mwanzo wa mimi kutoka, naweza kusema bila yeye nisingekuwa hapa leo hii.”

Una mchumba?
(Anakaa kimya kwa muda….)
“Mhhh, hapana! Kwa sasa sina na wala sihitaji kabisa kuwa naye hadi pale mambo yangu yakikaa sawa na kwanza mchumba huwa anatoka kwa Mwenyezi Mungu hivyo sina sifa ya kumchagua nani ananifaa.
“Na pia inategemea unaweza kuruhusu uhusiano ukashindwa kufanya mambo yako ya kimuziki vizuri.”

Una mipango ya kolabo la kimataifa?
“Yeah kila mwanamuziki wa sasa nchini anafikiria kusonga kimataifa zaidi. Nina mipango ya kuupeleka muziki huu mbali hususan huu ninaoimba (Reggae & Dance Hall).

“Ndoto yangu kubwa ni kufanya kolabo na staa wa Reggae wa kimataifa, Alaine.
Maua ameongea mengi kuhusiana na muziki, mahojiano kamili yatatoka hivi karibuni kupitia www.globaltvtz.com.


No comments

Powered by Blogger.