DONALD TRUMP AMTIBUA ADELE

Adele 

DIVA kutoka kiwanda cha muziki nchini Uingereza aliyegonga vichwa habari na kukonga nyoyo za mamilioni ya watu kote duniani kwa wimbo wake maararufu ”Hello”, Adele amekaririwa akisema kuwa hajatoa idhini yeyote kwa wimbo wake kutumika katika mikutano ya hadhara ya kufanyia kampeni za kisiasa nchini Marekani.
 
Donald Trump   
 

Kupitia kwa msemaji wake, Adele anasema kuwa,  japo Donald Trump  anayewania urais kwa kupitia Chama cha Republican kutumia wimbo wake uliotamba mwaka wa 2011 wa “Rolling in the Deep” katika mikutano ya hadhara katika jimbo la Iowa, lakini mwananasiasa huyo (Trump) hajaomba idhini kwa Adele.
Vile vile mgombea mwingine wa tikiti ya urais Mike Huckabee alitumia wimbo mpya kabisa wa Adele “Hello.” katika video moja ya kampeini yake iliyochapishwa kwenye mtandao wa Youtube.
“Adele hajatoa idhini ya mtu yeyote kutumia wimbo wake katika kampeni za kisiasa. Alisema kupitia barua pepe.
Hata hivyo barua hiyo haikubainisha iwapo mwanamuziki huyo huenda akachukua hatua za kinidhamu dhidi ya wale wote wanaocheza nyimbo zake bila Idhini.
Adele ambaye albam yake ya “25” ndiyo iliyouzwa sana nchini Marekani mwaka uliopita ndiye mwanamuziki wa pekee ambaye nyimbo zake zimetumika katika kampeini ya vyama vyote nchini Marekani.
Mwaka uliopita kundi la waimbaji wa muziki chapa Rock, R.E.M. walimuonya Trump dhidi ya kutumia nyimbo zao katika mikutano ya kisiasa.
Trump alikuwa ametumia wimbo waoa wa “It’s the End of the World”.
Isitoshe msanii mwingine Frankie Sullivan hakufurahishwa na matumizi ya wimbo wake uliovuma mwaka wa 1982 t “Eye of the Tiger,” katika mkutano wa wanahabari uliohudhuriwa na Kim Davis, wakala wa jimbo la Kentucky aliyefungwa jela kwa kukataa kutoa vyeti vya ndoa kwa wapenzi wa jinsia moja wanaofunga ndoa katika mji huo.

No comments

Powered by Blogger.