UJUE UNDANI WA SALUTI YA MAJI KWA VYOMBO VYA USAFIRI WA ANGA NA BAHARI

                                                                 New York Marekani
                                                             Addis Ababa, Ethiopia
                                                                      New York, Marekani
                                                             Dar es salaam, Tanzania
                                                                   Kisiwa cha Malta 
Na Sultani Kipingo 
Utamaduni huu umekuwepo kwa siku
nyingi, hata hapa Tanzania, lakini ujio wa moja ya ndege mbili aina ya
Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kutoka Canada ndio kumezua maswali
mengi kiasi hata ikabidi tufanye utafiti na kuja na majibu haya, maana upotoshaji na porojo vilitamalaki.

Kwa kawaida saluti ya maji (Water Canon
Salutation) iliyofanyiwa ndege hiyo Jumanne Septemba 20, 2016 katika uwanja wa
Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, hutolewa wakati wa
sherehe za chombo cha usafiri kinapoanza kazi kwa mara ya kwanza ama
kinapomaliza kwa mara ya mwisho.
Kwenye viwanja vya ndege magari ya Zimamoto husimama kila upande
wa njia ya kupitia ndege na kuinyunyizia itapopita chini yake, huku maji yakiwa
katika umbo la upanga wa sherehe kama ambavyo wanajeshi hufanya wakati za
harusi ya ofisa mwenzao.
Kwa mujibu wa utafiti wetu, saluti ya maji hutumika kumuaga
rubani mwandamizi aliyestaafu, mungoza ndege ama safari ya kwanza ama ya mwisho
ya ndege kwenye uwanja fulani ama ndege.
Saluti za maji hutumika pia hata kwa meli na vyombo vingine vya majini vinapoanza ama vinapomaliza kazi ama wakati wa kustaafu kwa nahodha
mwandamizi. 
Katika utafiiti wetu tumegundua kwamba
huu ni utamaduni wa kawaida kwenye bandari ama viwanja vya ndege ila sio sheria
ama lazima. Inasemekana ilianzishwa miaka ya nyuma katika bandari ya New York
nchini Marekani wakati wa kukaribisha meli.
Mfano mwaka 1962 melivita ya SS France
(baadaye ikaitwa Norway) ilipewa ukaribisho wa saluti ya maji, kitendo ambacho
kwa kuwa kilikuwa cha kuvutia kiliendelea kila mara meli ngeni ama mgeni mkubwa
akifika bandarini hapo.
Mwaka 1936 meli ya Unigereza RMS Queen
Mary ilipata mapokezi hayo.
Na mbali ya kuwa saluti ya maji kuwa ya
kusherehekea mwanzo ama mwishop wa chombo ama nahodha, zoezi hilo pia hutumika
kufanyia majaribio vifaa hivyo vya kuzimia moto.

No comments

Powered by Blogger.