PLUIJM: TUNGEKUWA MAKINI, TUNGEWANYOOSHA WAARABU NYINGI...
Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema walikuwa na nafasi ya kuimaliza Mo Bejaia ya Algeria kwa mabao mengi zaidi.
Yanga imeitwanga Mo Bejaia kwa bao 1-0 katika mechi ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Pluijm raia wa Uholanzi amesema walikuwa na nafasi nyingi za kufunga, lakini hawakuzitumia.
"Tungezitumia, basi lingekuwa jambo jema sana. Lakini hatukufanya hivyo," alisema.
"Ninaamini tuna kikosi kizuri, lakini bado tunahitaji kurekebisha mambo kadhaa, pia hilo suala la umaliziaji," alisisitiza.
Yanga imeitwanga Bejaia kwa bao la Thabani Kamusoko lililofungwa kwa kichwa kipindi cha kwanza akiunganisha krosi ya Juma Abdul.
Katika mechi ya kwanza kabisa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi, Yanga ililala kwa bao 1-0 ikiwa ugenini dhidi ya Bejaia.
Hii
ni mechi ya kwanza Yanga kushinda baada ya kucheza mechi tano, ikiwa
imefungwa tatu, sare moja na kushinda moja ambayo ni ya leo.
Sasa
Yanga ina pointi nne na inaendelea kubaki mkiani huku Bejaia inabaki na
pointi tano sawa na Medeama ya Ghana huku TP Mazembe ya DR Congo ikiwa
imejihakikishia kufuzu kwa kubaki kileleni na pointi 10.
Post a Comment