Mke wa Bilionea Msuya Kortini kwa Mauaji ya Wifi Yake
Dar es Salaam
MKE wa bilionea Erasto Msuya,
Miriam Elisaria Msuya (41) amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji
ya dada wa wa bilionea huyo, Aneth Msuya.
Mshtakiwa huyo alifikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana jijini Dar es Salaam na kusomewa
mashtaka na Wakili wa Serikali, Diana Lukondo mbele ya Hakimu Mkazi,
Margareth Bankika.
Akisoma mashtaka hayo, Lukondo alidai
mshtakiwa huyo ambaye ni mkazi wa maeneo ya Sakina kwa Iddi, jijini
Arusha anadaiwa Mei 25, mwaka huu katika maeneo ya Kibada Kigamboni
jijini Dar es Salaam alimuua Aneth Elisaria Msuya.
Mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote kwa
sababu mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji, mbapo
Jamhuri ilidai upelelezi haujakamilika na kuomba kesi hiyo ipangwe
tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Hakimu Bankika, alikubali kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 9, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na mshtakiwa alirudishwa rumande.
Habari zilizopatikana baada ya tukio
hilo zilidai kwamba, marehemu Aneth aliuawa kwa kuchinjwa na watu
wasiojulikana usiku wa kuamkia Mei 25, mwaka huu Dar es Salaam.
Mauaji hayo yalitokea nyumbani kwake
eneo la Kibada block 16, Kigamboni ambako inaelezwa wauaji hao
hawakuchukua kitu chochote ndani ya nyumba yake.
Marehemu Erasto Msuya, aliyekuwa
mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite aliuawa kwa kufyatuliwa risasi
Julai 7, mwaka 2013 katika eneo la Mijohoroni, kando ya barabara ya
Arusha – Moshi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, akiwa ameitika wito wa
kwenda kununua madini ya Tanzanite baada ya kupigiwa simu na vijana
wawili waliomtaka wakutane maeneo hayo.
Inaelezwa kuwa alifika katika eneo
hilo akiwa na gari lake aina ya Range Rover T 800 CKF na kuwakuta vijana
hao wakimsubiri, baada ya kuteremka Msuya alielekea kumsalimia mmoja wa
vijana hao.
Hata hivyo kabla hajamfikia kijana
huyo aliitoa bunduki ya SMG namba KJ 10520 aliyokuwa ameificha kwenye
koti na kumfyatulia risasi takribani 22 mwilini.
Post a Comment