Polisi: Marufuku Mikutano ya Ndani ya Kisiasa, Ishu ya Polisi 4 Waliouawa Benki Dar
KUFUATIA mauaji ya askari
wanne yaliyotokea Kata ya Mbande Temeke kwa watu wanaodhaniwa ni
majambazi kuvamia benki ya CRDB na kuwaua askari hao kwa kutumia silaha
za moto jeshi la Polisi limetangaza kiama na kuwataka wahusika wote
kujisalimisha.
Kauli hiyo imetolewa na Kamishna Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Nsato Marijan Mssanzya (CP), wakati akizungumza waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana ambapo pia alikiri kuwa mazoezi yanayofanywa na polisi yamelenga kukabiliana na Ukuta.
Akizungumza kwa hisia CP Mssanzya pia amepiga marufuku mikutano ya ndani yenye viashiria vya uchochezi na hata ikifanyika kwenye majukwaa watamshusha muhusika na kumfikisha kwenye mkono wa sheria.
Katika hatua nyingine jeshi la polisi
limehusisha tukio hilo na kile kinachoitwa Umoja wa Kupinga Udikteta
Tanzania (UKUTA) kufuatia matamko ya baadhi ya viongozi wa kisiasa ambao
wamesikika katika majukwaa ya kisiasa wakihamasisha wafuasi wao
wawashambulie askari wa Jeshi la Polisi.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na Kamishna Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Nsato Marijan Mssanzya (CP), wakati akizungumza waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana ambapo pia alikiri kuwa mazoezi yanayofanywa na polisi yamelenga kukabiliana na Ukuta.
Akizungumza kwa hisia CP Mssanzya pia amepiga marufuku mikutano ya ndani yenye viashiria vya uchochezi na hata ikifanyika kwenye majukwaa watamshusha muhusika na kumfikisha kwenye mkono wa sheria.
Amesema Jeshi hilo limebaini kwamba mikutano hiyo imekuwa
ikitumika kuchochea wananchi na kuwahamasisha kuvunja sheria za nchi na
kufanya mapambano na jeshi la polisi
“Kwasababu hiyo basi,kwa hali ya
kutumia mikutano ya ndani kuchochea watu kuvunja sheria na kupambana na
askari, hivyo basi kuanzia sasa jeshi la polisi nchini linapiga
marufuku mikutano yote ya ndani” amesema.
Aidha CP Mssanzya aliwataja askari
waliouawa katika tukio hilo wakati wakibadilishana lindo kuwa ni E.5761
CPL Yahya, F.4660 CPL Hatibu, G 9524 PC Tito na G 9996 PC Gastoni na
raia wawili waliojeruhiwa aliowataja kuwa Ali Chiponda na Azizi Yahya
wote wakiwa wakazi wa Mbande.
“Katika tukio hilo majambazi ambao
idadi yao haikufahamika walifanikiwa kupora silaha mbili aina ya MSG na
lisasi 60 na hakuna pesa wala mali ya benki hiyo kuibiwa au kuharibiwa,
ni dhahiri kuwa waharifu hao walikuwa na kusudio moja tu la
kuwashambiulia askari polisi, ” alisema.
Alisema katika hali ya kushangaza
baada ya tukio hilo kuna baadhi ya watu waliandika mitandaoni kubeza na
kukeji mazoezi ya kawaida ya jeshi la polisi na wengine waliandika
ujembe wa kushabikia tukio hilo la kuuawa kwa askari polisi huku wengine
wakidiriki kuandika ujumbe unaosema endapo watapigwa na polisi
Septemba1 mwaka huu basi viongozi wa jeshi hilo wawaondoe askari
wanaoishi uraiani na kuwarudisha kambini.
Aliongeza kuwa jeshi la polisi limejipanga vyema kukabiliana na matukio yote ya uvunjifu wa amani nchini
Post a Comment