LIONEL MESSI APAKA TATUU NYEUSI NUSU YA MGUU WAKE WA KUSHOTO

Mshambuliaji nyota wa Barcelona Lionel Messi amebadili uamuzi wake kuhusiana na tatuu ya kwenye mguu wake wa kushoto kwa kuuweka rangi nyeusi kwa sehemu kubwa.

Nyota huyo ambaye kwa sasa si jambo la kushangaza kutokana na kupenda tatuu, ameziba karibu michoro yote iliyokuwa kwenye mguu huo na kubakisha namba 10, mikono miwili pamoja na jina la mtoto wake Thiago.

Mabadiliko hayo ya tatuu katika mguu wa Messi yameonekana awakati akijiandaa kuivaa Brazil akiwa na timu ya taifa lake la Argentina katika mchezo utakaochezwa siku ya Alhamisi.
 Mguu wa Lionel Messi unavyoonekana sasa kama picha hii inavyoonyesha


No comments

Powered by Blogger.