PICHA 9: RAIS MAGUFULI ALIVYOENDELEA NA ZIARA YAKE IGUNGA NA NZEGA TABORA
Mkoani
Tabora, Rais Magufuli alizungumza na wananchi waliosimamisha msafara
wake katika vijiji vya Nanga na Ziba na alifanya mikutano ya hadhara
Igunga na Nzega ambako amewahakikishia wananchi kuwa serikali yake
itahakikisha inatekeleza ahadi zilizopo katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya
Mwaka 2015.
Katika
mkutano wa hadhara uliofanyika Igunga, Rais Magufuli amepokea
malalamiko ya wananchi kuhusu kutoanza kutumika kwa kituo cha mabasi na
soko na amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Tabora kuhakikisha kituo cha
mabasi cha Igunga na soko la Igunga vinaanza kutumika kuanzia Jumatatu
ijayo ya tarehe 01 Agosti, 2016.
Kuhusu
kero ya maji, Dkt. Magufuli alisema Tanzania imepata mkopo wa dola za
kimarekani Milioni 268.35 kutoka nchini India ambazo zitatumika
kutekeleza mradi wa kusambaza maji ya ziwa Viktoria katika Miji ya
Tabora, Igunga, Nzega, Sikonge
Rais
Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nanga Wilaya ya Igunga Masesa
Kishiwa Makala kutoka Chadema wakati akiwa safarini kuelekea Nzega
Mkoani Tabora.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
wabunge wa Mkoa wa Singida wakati akiwahutubia wakazi wa Misigiri Mkoani
Singida wakati akiwa njiani kuelekea Mkoani Tabora.
wabunge wa Mkoa wa Singida wakati akiwahutubia wakazi wa Misigiri Mkoani
Singida wakati akiwa njiani kuelekea Mkoani Tabora.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wakazi wa Misigiri Mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwasalimia wakazi wa Ziba Wilayani Igunga mkoani Tabora hawaonekani
pichani wakati akielekea Nzega Mkoani Tabora. PICHA NA IKULU
akiwasalimia wakazi wa Ziba Wilayani Igunga mkoani Tabora hawaonekani
pichani wakati akielekea Nzega Mkoani Tabora. PICHA NA IKULU
Post a Comment