MADAI: FLORA AMWANGUKIA MBASHA
Flora Mbasha
Stori: Erick Evarist, risasi jumamosi
DAR ES SALAAM: Habari ya mjini ni Mwimba Injili Bongo, Flora
Mbasha kudaiwa kumwangukia mumewe waliyetengana, Emmanuel Mbasha kwa kumuomba
radhi ndoa yao ichipuke upya kama zamani.
emmanuel Mbasha
Kwa mujibu wa mtoa ubuyu ambaye ni muumini wa Kanisa la
Evangelical Assemblies of God Tanzania (EAGT) ‘Mito ya Baraka’, Kariakoo, Dar
linaloongozwa na mchungaji Bruno Mwakibolwa, ambalo zamani wawili hao walikuwa
wakisali, baada ya jitihada za kurudiana kugonga mwamba, Flora alimfuata
mchungaji ili aweze kumsaidia arudiane na mumewe.
“Iko hivi, Flora awali alikuwa mzito kuomba radhi lakini
hivi karibuni aliamua kujisalimisha pale kanisani EAGT, akakutana na mchungaji,
akamuelezea matatizo yake.
“Mchungaji alimwambia
atalifanyia kazi suala hilo. Akamuita Mbasha (Emmanuel), akamhoji kwa saa tatu,
lakini hoja alizozitoa Mbasha, mchungaji mwenyewe alinyoosha mikono na
kumwambia awe huru,” alisema mtoa ubuyu huyo akiomba hifadhi ya jina lake.
“Mbasha alifunguka sana. Alimueleza kuwa, Flora alifikia
hatua ya kutamka kuwa mchungaji wake ni Gwajima. Sasa iweje leo amuone
Mwakibolwa?
“Pia Ima alimueleza mchungaji kuwa, Flora alizaa mtoto na
mwanaume mwingine wakati yeye ana matatizo. Flora huyohuyo alikomaa kuhakikisha
yeye anafungwa kwa kusimamia ile kesi ya ubakaji.
“Lakini pia, mara baada ya Mbasha kushinda kesi, Flora
alienda kukata rufaa japo alishindwa kwa kuchelewa muda wa kukata rufaa. Kwa
hoja hizo, mchungaji akaona hakuna jinsi zaidi ya kila mtu kuishi kivyake,”
alisema mtoa taarifa huyo.
Nje ya kanisa hilo juzi, paparazi wetu alikutana na mmoja wa
waumini aliyesema anaitwa Masasi ambaye alikiri Flora kufika kanisani hapo
kuongea na mchungaji lakini alidai hajui maongezi yao yalihusu nini.
Jitihada za kumpata mchungaji Mwakibolwa ziligonga mwamba
kwa kuambiwa alikuwa bize na majukumu ya huduma ya Bwana.
Alipotafutwa Flora ili aweze kuzungumzia suala hilo, simu
yake haikupatikana hewani lakini paparazi
wetu alifanikiwa kumpata Mbasha ambapo alipoelezwa ‘full’ stori, majibu
yake yalikuwa hivi:
“Nyie mmeipata hiyo? Aisee nyie kiboko, mko makini na
matukio. Labda mimi niseme tu hayo yalishapita, sipendi kuyazungumzia kwa sasa
maana nilishayasahau. Kwa sasa mimi namshukuru Mungu naendelea vizuri na
akipenda nitapata mwenzangu na nitawajulisha.”
Mwaka 2014, wawili hao walimwagana lakini miezi michache
mbele, Mbasha alipata kesi ya kudaiwa kumbaka shemejiye mwenye miaka 17.
Uhasama wao ulizidi, ikadaiwa Flora alikuwa nyuma ya kesi
hiyo. Mwaka jana, Mahakama ya Wilaya Ilala, ilimwona Mbasha hana hatia hivyo
kuwa huru na kila mmoja kuishi maisha yake huku Flora akisali Kanisa la Ufufuo
na Uzima kwa mchungaji Josephat Gwajima na Mbasha akisali Mito ya Baraka.
Post a Comment