CUF yagundua njama inayosukwa kuvunja ngome ya chama hicho kisiwani Pemba
Uongozi wa chama cha wananchi CUF kisiwani pemba umewataka wafuasi wa chama hicho kukaa mbali na mpango ulio gundulika wa kuleta mamluki ndani ya matawi ya chama hicho kisiwani pemba kwa lengo la kuivuruga ngome ya cuf kisiwani hapo.
Akizungumza na wandishi wa habari huko afisi ya wilaya chake chake katibu wa CUF wilaya chake chake Salehe Nassor Juma amesema mamluki hao wanaletwa kwalengo wananchi wachokozeke ilikuwapa nafasi mazombi ambao watakuja pamoja kuwapa sababu ya kuwapiga watu na kuwadhalilisha iliwananchi wapate woga.
Katibu Salehe amewataka vijana kisiwani pemba na zanzibar kwa ujumla kuto ingia katika mtengo hou unaoandaliwa ambao utapelekea kuwazalilisha wazee wanawake na watoto hivyo kuendelea kuwa wamoja katika kipindi hichi ambacho chama cha wananchi CUF kikiwa kina tafuta haki ya wazanzibar ya tarehe 25/10/2015.
Aidha katibu hyo amesema ugunduzi huo umemuonesha kuwa huenda kukafanyika kikao feki cha baraza kuu la uongozi taifa na kuwafukuza baadhi ya viongozi wakiwemo wabunge wa majimbo jambo mbalo linaweza kuharibu utulivu wawananchi walio nao hivi sasa hivyo amewataka wananchi.
Kufatia tarifa hio ilio tolewa na katibu huyo baadhi ya wafuasi wa chama hicho kisiwani pemba wamekuwa na maoni tafauti wengine wamekuwa wakitaka dola kuzisimamia katiba za vyama ilikuepuka uvunjifu wa amani huku wangine wakiweweseka na hali inavyo kwenda kwenye chama chao.
Post a Comment