Wabunge Waigomea Serikali.......Wakataa Kupangiwa Mishahara, Posho na Marupurupu
Wabunge
wamegomea hatua ya Serikali kutaka kusimamia posho na marupurupu yao,
huku wakitaka suala hilo waendelee kujipangia wenyewe.
Msimamo
huo uliotolewa na Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, umetolewa baada
ya Serikali kuwasilishwa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria
mbalimbali namba tatu ya mwaka 2016.
Awali
Serikali ilitaka suala la stahiki hizo kwa watumishi wa umma liamuliwe
na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora.
Akisoma
maoni ya Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohammed Mchengerwa,
alisema wametoa pendekezo hilo katika Sheria ya Utumishi wa Umma sura
298 kulinda dhana ya mgawanyo wa madaraka.
“Tume
ya Utumishi wa Bunge na Tume ya Utumishi wa Mahakama zipewe uhuru
kusimamia upangaji wa mishahara, posho na marupurupu mengine,” alisema.
Akizungumzia
mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, alisema kifungu cha 18 cha
Muswada huo kuhusu muda wa mnufaika kurejesha mkopo, Mchengerwa
alisema kamati inashauri mkopo uwe mwaka mmoja baada ya kumaliza masomo.
Alisema
hali hiyo itasaidia kutoa fursa kwa mnufaika kuanza kulipa mkopo
wake, utaratibu ambao hutumika katika nchi nyingine kama Kenya na
Zambia.
“Kuhusu
wanufaika waliojiajiri kamati inapendekeza kiwango cha kurejesha mkopo
kisipungue Sh 100,000 badala ya Sh 120,000 kama Serikali
ilivyopendekeza,” alisema Mchengerwa.
Awali,
akiwasilisha hotuba ya mabadiliko ya sheria hiyo, Mwanasheria Mkuu wa
Serikali (AG), George Masaju, alisema kifungu cha 8 cha Sheria hiyo
kinaanisha mamlaka ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais (Utumishi) kuwa ni
pamoja na kufanya uchunguzi kwa ajili ya kuendeleza ufanisi wa utumishi
wa umma.
Alisema
Ibara 24 ya Muswada huo inapendekeza kuongeza kifungu kipya cha 9A cha
Sheria kinachoweka masharti kuwa Taasisi, Wakala au Tume za Serikali
hazitakuwa na mamlaka ya kuidhinisha mishahara na marupurupu kwa
watumishi wa taasisi hizo na badala yake kibali kwa ajili hiyo
kitatolewa na Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais (Utumishi).
“Marekebisho
hayo yanalenga kuwa na mamlaka moja inayoratibu mishahara, posho na
marupurupu na watumishi katika taasisi za Serikali na pia kuwianisha
mishahara posho na marupurupu mengine kwa watumishi wa taasisi hizo.
“Masharti
yaliyopendekezwa hayatatumika. Ibara hiyo imefutwa na kuandikwa upya
masharti yanayopendekezwa hayatatumika kwa mishahara, marupurupu na
masilahi mengine kwa Bunge,Mahakama, Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ),Polisi,Magereza,JKT, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Idara ya
Usalama wa Taifa ili utaratibu huo kuendelea kama ilivyo sasa katika
sheria zinazosimamia taasisi hizo.
“Kifungu
cha 20 (1) (c) cha Sheria ya Utumishi wa umma kinaipa Tume ya Utumishi
wa Umma mamlaka ya kutunga kanuni kuhusu usaili wa watumishi wa umma
unaofanywa na tume hiyo,” alisema Masaju
Awali
kifungu cha 8 kilikuwa kinapendekeza kufanyiwa marekebisho kumpa
mamlaka Katibu Mkuu (Utumishi) kurekebisha na kuwianisha mishahara,
posho na marupurupu mengine kwa watumishi wa umma wakiwamo wabunge na
idara ya mahakama.
Huku
ikipendekeza kuongeza kifungu kipya cha 9A kinachozizuia taasisi za
umma, wakala, bodi na tume zisirekebishe au kuwianisha mishahara, posho
na marupurupu mengine kwa watumishi.
Sehemu
ya tano inapendekeza marekebisho katika Sheria ya Utumishi wa Umma,
Sura ya 298 kwa lengo la kutoa tafsiri ya neno “recruitment
secretariat”, maneno hayo yametumika katika Sheria lakini hayakuwa
yamepewa tafsiri.
Kiama kwa waajiri
Alisema
Ibara ya 19 ya Muswada huo, inapendekeza kufuta kifungu cha 20 na
21,ambacho kilikuwa kinaeleza kwa kuwa si rahisi mwajiri kufahamu kama
mtumishi anayeajiriwa ni mnufaika wa mkopo.
Kutokana
na hali hiyo,alisema Muswada unaainisha kuwa mwajiri atatakiwa
kuifahamisha Bodi ya Mikopo ndani ya siku 28,baada ya mwajiriwa huyo
mwenye Shahada au Astashahada ili bodi iangalie kama mwajiriwa huyo ni
mnufaika wa mikopo.
“Mwajiri
ambaye atashindwa kutekeleza masharti ya kifungu hicho atakuwa anatenda
kosa la jinai ambalo adhabu yake ni Sh milioni moja au kifungo cha
miezi sita gerezani. Pia inapendekezwa baada ya mnufaika wa mkopo
mwajiri atatakiwa kukata asilimia 15 ya mshahara wa mwajiriwa.
“Bodi
au mawakala wake wawe na mamlaka ya kukagua kumbukumbuku za waajiriwa
kwa lengo la kufuta taarifa zinazohusiana na wanufaika wa mkopo pamoja
na kumbukumbu za waajiriwa kwa lengo la kutafuta taarifa zinazohusiana
na wanufaika wa mkopo kwa hatua zao muhimu kuhusu makusanyo wa mikopo,” alisema
AG
Masaju alisema kifungu cha 57 cha sheria hiyo, kinaweka masharti kuhusu
zuio kwa shughuli za binadamu zinzoathiri ulinzi wa bahari, mito,
mabwawa zisifanyike ndani ya mita 60 kutoka kingo za bahari, mito au
mabwawa.
Alisema hatua hiyo imekusudiwa kuimarisha ulinzi na usalama wa mazingira ya maeneo husika ya bahari, maziwa na mito na mabwawa.
“Ibara
ya 11 ya Muswada inapendekeza kifungu hicho kirekebishwe katika kifungu
kidogo cha pili kuweka mwongozo wa namna ya kupima mita 60 ambako
shughuli za binadamu zimezuiliwa kufanyika.
“Kifungu
cha 184 kinaeleza athari na uthamini wa mazingira. Ibara ya 12
inapendekeza kuwa kitendo cha mtu yeyote kushindwa au kukataa kufanya
tathimini ya athari za Mazingira kwa mradi unaohitaji tathmini hiyo
kufanyika ni kosa la jinai ambalo adhabu yake ni faini isiyopungua Sh
milioni tano na isiyozidi Sh bilioni moja au kifungo kisichopungua miaka
miwili,” alisema.
Post a Comment