Taarifa kuhusu uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Uliofanywa na Rais Magufuli Leo
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe
25 Agosti, 2016 amemteua Bw. Andrew Wilson Massawe kuwa Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Kabla ya uteuzi huo Bw. Andrew Wilson Massawe alikuwa Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta katika Benki Kuu Tanzania (BOT).
Bw.
Andrew Wilson Massawe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Modestus
Francis Kipilimba ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya
Usalama wa Taifa.
Uteuzi wa Bw. Andrew Wilson Massawe unaanza mara moja.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
25 Agosti, 2016
Post a Comment