UVCCM yaivaa rasmi Chadema kwa kushindwa kufanya Maandamano ya UKUTA
Umoja
wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umewavaa viongozi wa Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kile walichodai kuendesha
siasa za maigizo baada ya kushindwa kuzindua Operesheni UKUTA, Septemba
1.
Kupitia
taaria yake kwa vyombo vya habari, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka
Hamdu Shaka, amesema kuwa Chadema walijua kuwa hawana ubavu wa kufanya
maandamano na mikutano nchi nzima Septemba 1 na kwamba walichofanya ni
kuwatia hofu wananchi.
“UVCCM
tulijua, tulielewa na kutambua bayana kwamba Chadema walikuwa wanafanya
maigizo katika siasa, hawana ubavu wala jeuri ya kuandamana kwa madai
ya kipuuzi na ambayo sio ya msingi kwa mustakabali wa nchi yetu,” alisema Shaka.
Aidha,
Shaka alikanusha sababu zilizotolewa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe kuahirisha maandamano hayo kuwa wameombwa na viongozi wa dini ili
waweze kukaa na pande zote kujaribu kutafuta suluhu kwa amani.
“UVCCM
inatamka bayana kuwa hakuna majadiliano, mazungumzo wala mijadala
itakayojadiliwa kati ya Serikali ya CCM na Chadema. Tunaomba Serikali ya
Rais John Magufuli iendelee na mikakati yake ya kisera,” Shaka ameongeza.
Kaimu
Katibu Mkuu huyo wa UVCCM alisisitiza kuwa Chadema hawana ubavu wa
kufanya maandamano na mikuano nchi nzima Oktoba 1 kama walivyosema,
baada ya kushindwa kufanya hivyo Septemba 1.
Shaka
amesema wanachokifanya hivi sasa Chadema kinatokana na kushindwa kubuni
mikakati ya kufanya siasa ili chama chao kiimarike na kukubarika.
Juzi, Chadema walitangaza kuahirisha uzinduzi wa oparesheni UKUTA nchi nzima, iliyokuwa imepangwa kufanyika jana (Septemba 1) kwa maandamano na mikutano nchi nzima.
UVCCM
pia walitangaza kuahirisha maandamano yao ya nchi nzima waliyokuwa
wamepanga kuyafanya Agosti 31 kwa lengo la kumpongeza Rais Magufuli kwa
kazi aliyoifanya ndani ya kipindi kifupi.
Maandamano ya pande zote mbili yalipigwa marufuku na Jeshi la Polisi nchini.
Post a Comment