GENK YAITAHADHARISHA TFF JUU YA SAMATTA

 Klabu ya Genk ambayo anacheza nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta, imetoa
tahadhari kwa benchi la ufundi la Taifa Stars hasa hususan upande wa
madaktari juu ya Mbwana Samatta ambaye ataungana na kikosi cha Mkwasa
moja kwa moja Lagos, Nigeria kwa ajili ya mchezo wa kukamilisha ratiba
ya kuwania kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika nchini Gabon
mwaka 2017.
Afisa habari wa TFF amethibitisha tahadhari hiyo waliyopewa juu ya
usalama wa Samatta katika mchezo huo.
“Kauli hii imekwenda sambamba na hali ya uchezaji wa mchezaji mwenyewe,
ambapo katika maelekezo wamesema wanaheshimu timu za taifa na wiki kwa
ajili ya michezo ya kimataifa ya FIFA”, Alfred alikiambia kipindi cha
Sports Extra cha Clouds FM.
“Genk wameshauri kwamba, kabla ya Samatta ahajacheza ni vizuri akapimwa
kwanza kwasababu alipewa majukumu mazito  ambapo alipewa mazoezi magumu
ya kuwa fit ili kuhakikisha anaisaidia timu yake kufuzu hatua ya makundi
ya michuano ya Europa League. Kwahiyo walitaka kuona anapata muda wa
kupumzika lakini imebidi wamwachie kwasababu anahitajika kwenye timu ya
taifa.”
Tanzania dhidi ya Nigeria utakuwa ni mchezo wa kukamilisha ratiba
kwasababu tayari Misri walmeshafuzu kutoka katika Kundi hilo la G.

No comments

Powered by Blogger.