Rais JPM Acharuka, Ataka Kuzibadili Noti


 Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli leo amekutana na kuzungumza na wahandisi katika mkutano wa 14 wa mwaka uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Katika kile kinachoonekana ni kutaka kuwadhibiti watu wanaodaiwa kuficha fedha, Rais Magufuli amesema kuwa mamlaka aliyonayo anaweza kuamua kubadili fedha ili zile zinazofichwa na watu hao wakose mahali pakuzipeleka.
Aidha amesisitiza kuwa katika utawala wake fedha za bure hazitakuwepo kwa sababu zilikuwepo awali zilitokana na fedha za wizi kutoka serikalini ambazo kwa sasa zimedhibitwa, alisema kwa mwendo anaokwenda nao sasa sasa ni ngumu kwa mwananchi kupata fedha bila kufanya kazi.

No comments

Powered by Blogger.