Hukumu Kesi ya Babu Tale Yaahirishwa Tena
HUKUMU ya kesi inayomkabili Meneja wa
Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Babu Tale, ya kusambaza na kuuza
DVD za mawaidha ya Shehe Hamis Mbonde bila ridhaa yake imeahirishwa tena
leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam mpaka Septemba 12, mwaka
huu.
babu tale na diamond
Kwa mujibu wa Msajili wa Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam, Mustapha Sian alisema sababu kubwa ya
kuahirishwa kwa kesi hiyo ni kwamba aliyetakiwa kuitolea hukumu ambaye
ni Msajili Projest Kahyoza hayupo mahakamani kikazi.
Katika kesi hii Babu Tale, pamoja na
mdogo wake anayeunda kundi la Tip Top Connection wanatakiwa kuieleza
mahakama kwa nini wasifungwe jela ama kumlipa Shehe Mbonde kiasi cha Sh.
Milioni 250.
Post a Comment