Majambazi Yaua Polisi 3 Mbagala, Dar
ASKARI polisi watatu wameuawa kwa kupigwa na raisasi na majambazi huko Mbagala, Mmbande jijini Dar es Salaam usiku huu.
Inadaiwa kuwa askari hao walikuwa
wakibadilishana lindo katika Benki ya CRDB, tawi la Mbagala Mmbande na
mara wakaibuka watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi na kuanza
kuwashambulia kwa risasi na baada ya shambulizi hilo wanadaiwa kuondoka
na pikipiki wakielekea maeneo ya Mvuti.
Polisi waliouawa ni pamoja na;
E5761 CPL YAHAYA
F4660 CPL HATIBU
G9544 PC TTITO.
Inasemekana kuwa tukio hilo limetokea
mnamo saa 1: 30 usiku katika na inadaiwa kuwa wahalifu hao waliondoka na
silaha moja aina ya SMG.
Mmoja kati ya polisi waliouawa alikuwa
anaingia lindo, mmoja alikuwa anatoka na mwingine alikuwa dereva na
imeelezwa kuwa majambazi hayo hayakuingia ndani ya benki ila gari la
polisi (Leyland Ashok) limeharibiwa kwa risasi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Simon Sirro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo: “Ni kweli
kumetokea tukio la uvamizi hapa Mbagala lakini taarifa kamili nitazitoa
kesho kwa kuwa bado nipo eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi”.
Alisema Kamanda Sirro.
Post a Comment