Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta ametumia kiasi cha
milioni 130 kununua gari yake ya kwanza nchini Ubelgiji. Ameweka picha
kwenye akaunti yake ya mtandao wa Twitter na kuandika maneno ya
kumshukuru Mwenyezi Mungu, ‘Thanks God’.
Hili ndilo gari jipya la Mbwana Sammata.
Gari hilo alilonunua mchezaji huyo ni Benz Cla220 Cdi AMG Sport 2016 ambayo gharama yake inadaiwa kuwa ni €46,680.
Samatta amechukua uamuzi huo baada ya kufanikiwa kupata leseni inayomruhusu kuendesha gari nchini humo
|
Muonekano wa nyuma wa gari hilo.
Inadaiwa kuwa mchezaji huyo analipwa kiasi cha €35,600 kutokana na
mkataba wake wa kuichezea timu ya Genk ambao utamalizika mwaka 2020.
Kwa sasa Samatta ameonekana kuwa miongoni mwa wachezaji wa kutegemewa
kwenye timu ya KRC Genk ambayo inashiriki kwenye michuano ya Europa
League pamoja na ligi kuu nchini Ubelgiji japo amekuwa nje ya uwanja kwa
wiki mbili akiuguza majeraha. |
Post a Comment