Makamu Wa Rais Kuongoza Upandaji Miti leo Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam Paul Makonda.
MAKAMU wa Rais, Samia Hassan Suluhu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji Miti Mkoa wa Dar es Salaam.
uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji Miti Mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar jana, mkuu wa mkoa huo,
Paul Makonda amesema kila mwananchi wa Dar anapaswa kupanda mti mmoja
kwa ajili ya ustawi wa afya na mazingira.
Amesema zoezi hilo litazinduliwa rasmi na Samia Suluhu katika
Barabara ya Kilwa kwenye Wilaya ya Temeke na baadaye watakagua
miundombinu
ya maji kwa ajili ya umwagiliaji wa miti hiyo.
ya maji kwa ajili ya umwagiliaji wa miti hiyo.
Makonda amesema miti hiyo itakayopandwa ni faida ya Mkoa wa Dar kwa
ajili ya hewa pamoja na vivuli vya kupumzika hivyo amewataka wananchi
kupanda miti yao katika maeneo yanayowazunguka pamoja na
watendaji wote wa mitaa na kata wa mkoa wa Dar.
watendaji wote wa mitaa na kata wa mkoa wa Dar.
Na Denis Mtima/GPL.
Post a Comment