Diamond: Nimenunua nyumba SA, nimechoka kuhangaika hotelini
Baada ya kudai kuwa ana nyumba Afrika Kusini na haoni sababu ya kununua
nyumba nchini Marekani , Diamond amefunguka sababu iliyomfanya anunue
nyumba nchini humo.
Mapema mwezi April mwaka huu, alipohojiwa kwenye Stori Tatu ya Planet Bongo, inayoruka kupitia EA Radio, Diamond alisema, “Sina sababu ya kusema ninunue nyumba Marekani. Ninunue nyumba Marekani kwa sababu gani? Kwanza sipapendi, uongozi unajua kabisa.”
Akiongea na Times FM, hitmaker huyo wa ‘Kidogo’ amesema kuwa sababu iliyomfanya yeye kununua nyuma Afrika Kusini ni kutokana na kuchoka kuhangaika kwenye hoteli kupanga wakati anapokuwa nchini humo.
“Mimi mwenyewe kwanza nipate urahisi wa makazi nikiwa kule, nimechoka kuhangaika mahotelini,” amesema Diamond. “Lakini familia yangu ipo kule, mwanangu Tiffah na mwingine ambaye anakaribia kuja kwahiyo nawawekea mazingira bora wasije kuona kwamba baba anazalisha tu.”

Post a Comment