Exclusive: Vijana Waiba Baraghashia ya Mzee Akilimali, Achimba Mkwara Mzito
Mzee Ibrahim Akilimali maarufu kwa jina la Mzee Akilimali.
Taarifa zilizotufikia ni kuwa Mzee Ibrahim Akilimali maarufu kwa jina
la Mzee Akilimali ambaye ni katibu wa Baraza la Wazee wa Klabu ya
Yanga, amelalamika kuwa kofia yake aina ya baraghashia imeibiwa na mtu
ambaye hajajulikana.Baada ya kuibiwa Mzee Akilimali ametoa mkwara mzito kwa yeyote ambaye amehusika kuiiba kofia hoyo ambayo muda wote amekuwa akionekana hadharani ameivaa.
Mtu wa karibu wa Mzee Akilimali amesema kuwa mzee huyo alikutwa na mkasa huo jana alipokuwa ameenda kumtembelea mzee mwenzake aliyemtambulisha kwa jina la Mzee Mwika.
“Sasa alipofika pale wakawa wamekaa wanapiga soka za hapa na pale, baada ya muda wakatengewa chain a vitumbua lakini Mzee Akilimali yeye huwa anapendelea mihogo na siyo mlaji wa vitumbua, akiwa amevua kofa yake, akaenda jirani kununua mihogo,” alisema mtu huyo wa karibu na mzee huyo.
Mtu huyo wa karibu akaendelea kusimulia kuwa: “Aliporejea hakuikuta kofia yake hata mzee mwenaake hakujua ilipoteaje, basi katulia akaendelea kunywa chai huku akitoa mkwara kuwa ole wake aliyeiiba.”
Alipotafutwa Mzee Akilimali mwenyewe alikiri kutokea kwa tukio hilo kwa kusema: “Ni kweli na nimesikia kuna kijana fulani aliiba na tulipoiulizia tuliambiwa tayari ameshaiuza, ila namtaka arejeshe kwa hiyari yake mwenyewe,” alihitimisha mzee huyo bila kutaka kufafanua zaidi.
Post a Comment