ALIYEPIGA PICHA MAUAJI YA MWANGOSI AFARIKI DUNIA
Mpiga picha wa Gazeti la Tanzania Daima, aliyepiga picha za
tukio la mauaji ya Mwangosi Joseph Senga enzi za uhai wake.
Na Dotto Bulendu
Na Dotto Bulendu
NI simanzi na majonzi, siku moja baada ya Mahakama Kuu Kanda
ya Iringa kumhukumu kifungo cha miaka 15 askari aliyemuua mwandishi Daudi
Mwangosi, tasnia ya habari imepata pigo kwa kuondokewa na mpiga picha wa Gazeti
la Tanzania Daima, aliyepiga picha za tukio la mauaji ya Mwangosi, SHUJAA
JOSEPH SENGA, aliyefariki dunia jana usiku.
Senga amefia nchini India alikopelekwa kwa matibabu ya
ugonjwa wa moyo.
Mojawapo ya picha za tukio la mauaji ya Mwangosi alizopiga
Joseph Senga.
Bila Joseph Senga, shujaa aliyehatarisha maisha yake,
akasimama bila woga, akapiga picha akiwa katikati ya msitu wa askari polisi
wenye silaha, huku anga ikiwa imegubikwa na moshi wa mabomu ya machozi, milio
ya risasi ikisikika na kuzitunza, zikasaidia kufichua mauaji ya Mwangosi, leo
hii asingekuwa Senga, nadhani kusingekuwa na kesi na mwisho hukumu dhidi ya
aliyemuua Mwangosi. Nakulilia Senga.
Daudi Mwangosi enzi za uhai wake.
Senga, Senga, Senga, Senga, umekwenda, Mungu aliamua akuweke
hai mpaka hukumu itoke na mwisho amekuchukua, Senga umekwenda wadogo zako
katika tasnia tukiwa na hamu ya kujifunza kutoka kwako.
Senga, Senga, kamsalimie Daudi Mwangosi, mwabie aliyemuua
naye kahukumiwa jela miaka 15, kamwambie mazingira ya waandishi wa habari bado
magumu.
Nenda Senga, picha zako zinabaki kuwa rejea ya mafunzo ya
uandishi wa habari katika mazingira hatarishi.
Post a Comment