Serikali yampa Gwajima masharti ya kuingiza ndege yake nchini
Siku moja baada ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Joesphat Gwajima kusema kuwa ataileta Tanzania ndege yake binafsi, Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imekana kuwa na taarifa kuhusu ujio wa ndege hiyo.
Ofisa Habari wa TCAA, Ali Changwila alisema kuwa hawana taarifa kwamba Askofu Gwajima ana mpango wa kuingiza ndege yake nchini.
Juzi Askofu Gwajima alithibitisha kununua ndege hiyo aina ya Gulfstream N60983 yenye thamani ya Tsh 2.64 kwa ajili ya kuendeleza ufalme wa Mungu.
Askofu Gwajima aliweka picha katika ukurasa wake wa Instagram akiwa amesimama mbele ya ndege hiyo ambapo alisema karibuni itawasili Tanzania kwa ajili ya shughuli zake za injili.
TCAA imesema kuwa Mtanzania yeyote anayenunua ndege nje ya nchi na kutaka kuiingiza nchini anatakiwa kwanza kuitaarifu mamlaka hiyo ili iweze kuwa na taarifa kamili. Aidha, alisema kabla ndege hiyo haijaingizwa nchini ni lazima wataalamu wa TCAA wajiridhishe kuwa wanaifamahu na ifanyiwe ukaguzi.
TCAA imesema ndege hukaguliwa kabla haijaingizwa nchini ili kujirisha kuwa inakidhi vigezo vya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO).
Mbali na vigezo hivyo, wanakagua pia kama ina vyeti vya usajili, historia yake, imekwisha muda wake? imeshakatazwa kusafiri? Ukaguzi wote huo ni kuepuka kutumia ndege ambayo muda wake wa matumizi umepita, kwani baadhi ya watu huuza ndege ambazo muda wake wa kutumia umekwisha.
Baada ya wataalamu kujiridhisha na vyote hivyo, ndege hiyo itatakiwa kujaza fomu ya TCAA ili iweze kufuata sheria za nchi ambapo itaelezwa itarushwa na rubani gani na itatumia viwanja gani.
Post a Comment