TAMBWE ATIMKA YANGA USIKU MNENE

       Amissi Tambwe.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Yanga, Amissi Tambwe, juzi usiku aliondoka nchini kwa siri na kwenda nchini Kenya bila ya uongozi wake kuwa na taarifa.
Inadaiwa kuwa Tambwe ilienda huko kwa ajili ya kuonana na wakala wake ambaye hapo awali alikuwa akimtafutia timu ya kucheza katika mataifa ya Kiarabu kabla ya hajaongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Yanga hivi karibuni.
Baada ya Championi Jumatatu kupata taarifa hizo zilizoibuka wakati dirisha la usajili likielekea kufungwa, usiku wa jana, lilimtafuta Tambwe bila ya mafanikio kutokana na simu yake ya mkononi kutokuwa hewani.
Hata hivyo, mmoja wa rafiki zake wa karibu aliliambia gazeti hili kuwa: “Ni kweli Tambwe ameenda Kenya na lakini sijui kaenda kwa ajili ya kazi gani. Lakini ninachohisi atakuwa ameenda kuonana na wakala wake kwa ajili ya kuweka mambo yake sawa kwani kabla ya kuongeza mkataba Yanga alikuwa akimtafutia timu katika mataifa ya Kiarabu,” alisema rafiki yake huyo.

No comments

Powered by Blogger.