Nilifanya upumbavu ujauzito wangu
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ruby ambaye hivi karibuni aliibua hali ya sintofahamu mitandaoni baada ya kupost picha akionyesha tumbo lake na wengi kuhisi ni mjamzito, amesema aliamua kufanya upumbavu kuhusu tukio hilo.
Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na East Africa Television na East Africa Radio, Ruby amesema hana ujauzito kabisa isipokuwa picha zilizoonekana akiwa na kitumbo alilitunisha tu.

"Actually hii itaonekana kama upumbavu sijui, ila niliamua tu kulitunisha tu tumbo langu, na si unajua Watanzania wanavyopenda ubuyu!! Ila sio mjamzito", alisema Ruby.
Ruby ambaye kwa sasa yupo kwenye mahusiano na kijana anayejulikana kwa jina la Genely Hb, kwa mara ya kwanza ameweka mahusiano yake wazi na kijana huyo, ambaye inasemekana alishawahi kugombana na wasichana wengine kwa ajili yake.
Baadhi ya picha ambazo Ruby alipost na kuibua gumzo la kuwa na ujauzito. |
Post a Comment