RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA RAIS MUSEVENI WA UGANDA WAWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA HOIMA UGANDA MPAKA BANDARI YA TANGA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake, Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga huku viongozi mbalimbali wa Tanzania na 
Uganda wakishuhudia. Shughuli hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono wa pongezi na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga huku Viongozi mbalimbali wa Tanzania na 
Uganda wakishuhudia. Shughuli hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimueleza jambo Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la Mradi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania.
 Baadhi ya wananchi wakifurahia jambo wakati wa hotuba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la Mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania.
 Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimpa mkono Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumaliza kuhutubia katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga 
Nchini Tanzania.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mbalimbali waliohudhuria shughuli ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda 
hadi Tanga katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati wakielekea kuweka jiwe hilo la msingi. 
Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika sherehe hizo za uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa bomba la mafuta.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii mbalimbali mara baada ya kutumbuiza.
 Rais wa Uganda Yoweri Museveni akihutubia katika viwanja vya Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga. PICHA NA IKULU.

No comments

Powered by Blogger.