YANGA KUTEST MITAMBO LEO DHIDI YA SINGIDA UNITED, CHIRWA KUIKOSA MECHI

Yanga inatarajiwa kushuka uwanjani leo kukipiga dhidi ya Singida United katika mchezo wa kirafiki kujiandaa kwa ajili ya msimu ujao.
Timu hizo zinakutana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam lakini Yanga itawakosa viungo washambuliaji  Obrey Chirwa raia wa Zambia na mzawa Geoffrey Mwashiuya kutokana kusumbuliwa na maumivu.
Msemaji wa Yanga, Dismas Ten amethibitisha juu ya hilo kwa kusema wachezaji wengine wote wapo vizuri kuelekea mchezo huo wa kwanza wa timu hiyo kujipima nguvu baada ya maandalizi ya msimu mpya kwa takriban mwezi mmoja.
Ten amesema viingilio katika mchezo huo vitakuwa ni Sh 15,000 kwa VIP A, Sh 10,000 kwa VIP B na C na majukwaa mengine yote yaliyosalia itakuwa ni Sh 3,000.

No comments

Powered by Blogger.