Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema aswekwa mahabusu kwa mahojiano zaidi.
Mbunge
wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, amesafirishwa kutoka Mkoani
Dodoma usiku wa kumkia jana na kuswekwa kwa mara nyingine tena Mahabusu
Mkoani Arusha kwa mahojiano ya kutoa lugha za uchochezi.
Akizungumza
leo na waandishi wa habari ofisini kwake , Kamanda wa Polisi Mkoani
Arusha, Charles Mkumbo, amesema Lema wamemweka mahabusu mpaka
watakapomaliza mahojiano.
Amesema kuwa endapo watamaliza mahojiano atafikishwa mahakamani wakati wowote, ili kujibu makosa anayokabiliwa nayo.
Mkumbo amesema Lema amekuwa akitoa maneno na lugha za uchochezi na kuzirudia kila mara, hivyo wameona vema wamweke ndani.
Amesema juzi walimkamata na kumuhoji, kisha kumwachia kwa dhamana, lakini kuna baadhi ya makosa hakuhojiwa, na ndiyo wanamuhoji.
Aidha licha ya kumkamata Lema na kuendelea kumuhoji, lakini hakutaja maneno yapi na lugha za uchochezi alizotoa Mbunge huyo.
Novemba
Mosi mwaka huu, Kamanda Mkumbo akiwa anazungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake, alitaja maneno ya uchochezi anayodaiwa Lema kutaja kuwa
ni: “Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania akiendelea
kukandamiza demokrasia,siasa za ukandamizaji taifa litaingia katika
umwagaji wa damu,nchi hii inaandaliwa kwenda katika utawala wa
kidikteta,”
Post a Comment