REAL MADRID YANG'ANG'ANIA KILELENI MWA LIGI YA LA LIGA

 Real Madrid imeendelea kung'ang'ania kileleni mwa ligi ya La Liga baada ya kuchapa wachovu Legene kwa magoli 4-2.
James Rodriguez aliifanya Real Madrid iongoze kwa kutumbukiza wavuni mpira, kabla ya Morata kufunga la pili kwa kichwa na kuongeza la tatu kwa shuti kali.
Leganes walijibu mapigo kwa kufunga kupitia kwa Gabriel na kuongeza lingine kupitia kwa Luciano, lakini mpira wa kichwa wa Morata ukaifanya Real kupata
goli la nne.
                                          James Rodriguez akishangilia goli la kwanza alilofunga
                                  Alvaro Morata akifunga goli la pili kati ya matatu aliyoyafunga jana

No comments

Powered by Blogger.