Nape Nnauye Kuanika Ukweli Wote Jumamosi Hii
Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema kuwa Jumamosi April 8, 2017 atakuwa jimboni kwake ambapo atazungumza na wapiga kura wake kuwaeleza ukweli wa mambo yaote yaliyotokea.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Nape Nnauye amendika kuwa, “Shukrani
kwa wote mlioniunga mkono katika kusimamia haki. Narudi Mtama kuwaeleza
wapiga kura wangu UKWELI WOTE. Ni Jmosi hii tar 8/4/17.”
Nape
aliondolewa kwenye nafasi hiyo wiki chache zilizopita baada ya kupokea
taarifa ya Kamati ya Uchunguzi ya Saa 24 aliyoiunda kufuatia Kituo cha
Clouds TV kuvamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Nape
aliahidi kupeleka ripoti hiyo kwa wakuu wake ambao ni Waziri Mkuu,
Makamu wa Rais na Rais John Pombe Magufuli ambapo siku iliyofuata Rais
alitengua uteuzi wake na kumteua aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria,
Dkt. Harrison Mwakyembe kuchukua nafasi ya Nape.
Post a Comment