MVUA YALETA MADHARA NA KUSABABISHA KAYA 20 KUKOSA MAKAZI

 Baadhi ya Nyumba katika eneo la Chalinze Mzee zikiwa zimearibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiangalia madhara yaliosababishwa na mafuriko katika jimbo hilo la Chalinze.
 wakazi wa chalinze wakiangalia nyumba zao zilizobomoka kutokana na mafuriko.
 Sehemu ya bwawa la umwangiliaji la Msoga liloaribiwa na mafuriko na kupasua kingo za bwawa hilo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete (mwenye kanzu) akiwa na wananchi wa jimbo hilo wakikagua `Bwawa la Umwangiliaji la Msoga
 Moja ya Nyumba iliyobomoka kutoka na mvua zinazoendelea kuonyesha katika eneo la Chalinze.
  Moja ya Nyumba iliyobomoka kutoka na mvua zinazoendelea kuonyesha katika eneo la Chalinze.
 Moja ya Nyumba iliyobomoka kutoka na mvua zinazoendelea kuonyesha katika eneo la Chalinze.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akisaini kitabu katika Ofisi za kijiji cha Msoga.
 

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete,ametembelea eneo la Chalinze Mzee lilokumbwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika jimbo hilo na kusababisha madhara ya nyumba kubomoka na nyumba 9 kusombwa na maji na kusababisha zaidi ya kaya 20 kukosa pakulala.

Akizungumza Ridhiwani,ametaja maeneo yaliyokumbwa na mafuriko ni Chalinze Mzee,Bwawa la umwangiliaji la Msoga ambalo limetoboka na shule ya Sekondari ya Imperial.

Aidha,amesema kuwa madhara makubwa yaliosababishwa na mafuriko hayo ni kuharibika kwa mashamba,nyumba za wananchi kuharibika na kusabbishwa wananchi kukosa pa kulala,na ameongeza kuwa kwasasa wananchi hao wanahitaji msaada.

Ridhiwani ametoa pole kwa wakazi hao na kuwaomba kuwa vumilivu katika kipindi hiki.

No comments

Powered by Blogger.