BREAKING NEWS: Majambazi Waua Polisi Watatu Mkuranga

Habari zilizotufikia hivi punde, zimeeleza kuwa, askari polisi watatu wameuawa na majambazi huko Mkuranga, Mkoani Pwani.
Habari hizo zinasema kuwa, askari hao wameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi hao wakati wakijiandaa kuondoka kwenye lindo ambalo lilikuwa ni kizuizi cha barabarani ili warudi kituoni.
Imeelezwa kwamba majambazo hao waliwavamia ghafla polisi hao waliokuwa kwenye gari na kuwapiga risasi na kuwaua wote palepale eneo la tukio, kisha kutokomea kusikojulikana.
Habari zaidi tutawaarifu baadaye kadiri tutakavyozipata.
 

No comments

Powered by Blogger.