Maalim Seif Azuiliwa na Jeshi la Polisi Kufanya Mkutano wa Ndani Mtwara
Vingozi wa CUF wakisalimiana na Jumuiya ya Vijana ya CUF (JUVICUF).
Viongozi wa CUF wakiongea jambo na Maalim Seif.
MTWARA: Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif,
leo alialikwa kuhudhuria mkutano wa ndani wa chama ulioandaliwa na
Jumuiya ya Vijana ya CUF(JUVICUF) Mtwara Mjini, kama mgeni rasmi. Kwa
taarifa za uhakika ni kuwa Jeshi la Polisi wadaiwa kuipokea barua ya
Jumuiya ya Vijana ya CUF(JUVICUF ) na kuijibu wakiruhusu Mkutano huo
uendelee na kwamba wangeulinda. Jana, Polisi pia walikabidhiwa barua ya
Katibu Mkuu wa CUF kwenda kwa IGP na ma RPC Lindi na Mtwara akiwajulisha
juu ya ziara yake.
Mapema leo wakati Maalim Seif akitua Mtwara Mjini , Polisi
wamekwenda na magari yao na vitambaa vyekundu na kuzingira ukumbi wa
kikao huku watu wakifukuzwa. Kisha Polisi wakawapa viongozi wa CUF barua
nyingine ya kutengua ile barua ya ruhusa.
Post a Comment