Majuto: Nataka Nikifa Nizikwe Kama Steven Kanumba
NA IMELDA MTEMA | RISASI JUMAMOSI:
Wiki hii, Mpaka Home ilifunga safari mpaka mkoani Tanga, nyumbani kwa mchekeshaji maarufu wa siku nyingi, mzee Amri Athumani (68) ‘Mzee Majuto’ kwa lengo la kuyajua maisha halisi ya mchekeshaji huyu.
Mzee Majutoakifanya usafi nyumbani.
Majuto: Kwa nini nisizae bado nina nguvu lakini kwa mke
wangu si kwa mwanamke mwingine na wala siwezi kumkufuru Mungu kwa
kukatiza kufanya hivyo.
Mpaka Home: Ulienda kuhiji Makha ni tofauti gani uliyonayo kabla hujaenda huko na baada ya kurejea?
Majuto: Jamani mimi wengine ni mashabiki zangu tu umri wangu huu natafuta nini tena jamani, siwezi maana unakuta wengine wanataka kupiga picha hivyo siwezi kukataa kupiga picha na mashabiki hata mara moja maana nataka siku nikizikwa na mimi nizikwe kama Kanumba lakini hakuna kingine.
Mpaka Home: Nimeona umevuna mahindi, mihogo umeviweka hapa nyumbani vipi bado unalima?
…wakiandaa makopa na mkewe jikoni.
Mpaka Home: Nini kinakufurahisha unapokuwa nyumbani kwako?
Wiki hii, Mpaka Home ilifunga safari mpaka mkoani Tanga, nyumbani kwa mchekeshaji maarufu wa siku nyingi, mzee Amri Athumani (68) ‘Mzee Majuto’ kwa lengo la kuyajua maisha halisi ya mchekeshaji huyu.
Mzee Majutoakifanya usafi nyumbani.
Mzee Majuto anaishi eneo linaloitwa
Donge, mkoani humo ambapo anaishi na familia yake nzima akiwepo mkewe
kipenzi; Asha, watoto wake pamoja na wajukuu wake. Mcheshaji huyu
ameyaweka wazi maisha yake halisi kama ifuatavyo:
Mpaka Home: Kwa nini umeamua kuishi mkoani wakati mastaa wengi wanapenda kuishi Dar es Salaam?
Majuto: Mimi sipendi
fujo kabisa, napenda kutuliza akili yangu sasa huko Dar ni vurugu tupu.
Siwezi kukaa huko bora niishi hukuhuku atakayeniona mimi mshamba shauri
yake.
Mpaka Home: Nimemuona mtoto mdogo hapa nimesikia akikuita baba kumbe bado unazaa?
Mpaka Home: Ulienda kuhiji Makha ni tofauti gani uliyonayo kabla hujaenda huko na baada ya kurejea?
Majuto: Tofauti ni
kubwa sana kwa sababu nyumba yetu imekuwa ni nyumba ya ibada wakati wote
na tunaishi kwa amani, ugomvi hakuna kama zamani.
Mpaka Home: Unapokuwa nyumbani unapenda mama akutayarishie nini?
Majuto: Napenda sana ugali wa muhogo na samaki ndiyo chakula changu kikubwa na ninakifurahia.
Mpaka Home: Kila mtu ana kitu chake kinachomvutia anapokuwa nyumbani kwake, wewe unavutiwa na nini?
Majuto: Napenda sana nikiwa nyumbani nikae jikoni na mke wangu tunapika na kupiga stori huku chakula kinaiva.
…akiwa na mjukuu (kushoto) pamoja na mtoto wake.
Mpaka Home: Hapana nyumbani nawaona watoto wengi sana wote ni watoto wako?
Majuto: Hapana wengine ni wajukuu zangu tena nawapenda sana.
Mpaka Home: Mara nyingi kumekuwa na tuhuma kuwa unapenda kuoa dogodogo angali una mke wako, vipi hilo?Majuto: Jamani mimi wengine ni mashabiki zangu tu umri wangu huu natafuta nini tena jamani, siwezi maana unakuta wengine wanataka kupiga picha hivyo siwezi kukataa kupiga picha na mashabiki hata mara moja maana nataka siku nikizikwa na mimi nizikwe kama Kanumba lakini hakuna kingine.
Mpaka Home: Nimeona umevuna mahindi, mihogo umeviweka hapa nyumbani vipi bado unalima?
…wakiandaa makopa na mkewe jikoni.
Majuto: Kwanza mara
nyingi mimi siishi hapa mjini naishi zangu shamba huko Kiruku, nje
kidogo ya jiji kuna kila aina ya vitu ufugaji na bado nalima na pia
nimejenga msikiti hukohuko shamba kwa ajili ya kuswali.
Mpaka Home: Ni kitu gani umefaidika katika kipindi chote cha uigizaji wako?
Majuto: Unajua mimi nimefanya mambo mengi kupitia
jitihada zangu inawezekana ningekuwa mbali sana lakini watu wengi
wamenidhulumu jasho langu ila kwa vile sipendi kumdai mtu nimemuachia
Mungu maana ningeweza hata kuwa msanii wa kwanza kwa utajiri hapa
Tanzania. Hivi nilivyonavyo, nyumba na mambo mengine ni vitu vidogo tu.Mpaka Home: Nini kinakufurahisha unapokuwa nyumbani kwako?
Majuto: Ni familia yangu na kuwa karibu na mke wangu.
Mpaka Home: Ni kitu gani unatamani kiwe hapa nyumbani kwako na hakipo?
Majuto: Natamani sana nyumba yote iwe imezungukwa na miti maana napenda sehemu yenye hewa safi na nzuri. Nitapanda.
Post a Comment