ARSENAL YAZINDUKA NA KUICHAPA WEST HAM MAGOLI 3-0

 Arsenal imefufua matumaini ya kutinga Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani baada ya kupata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya West Ham na kukwea hadi nafasi ya tano katika Ligi Kuu ya Uingereza. Baada ya kipindi cha kwanza ambacho hakikushuhudia goli, Mesut Ozil akiichezea Arsenal kwa mara ya 150 aliifungia goli la kwanza kufuatia makosa ya kutomiliki mpira ya Jose Fonte. Ozil aligongeana vyema na Alexis Sanchez na kumtupia krosi Theo Walcott ambaye alikuwa kapteni kufuatia Laurent Koscielny, ambaye hakufanya ajizi na kufunga goli. Olivier Giroud aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Alex Oxlade-Chamberlain, alipiga shuti la kuzungusha na kufunga goli la tatu.
                                        Mesut Ozil akiwa ameupiga mpira uliozaa goli la kwanza
                          Olivier Giroud akipiga shuti la kuzungusha na kufunga goli la tatu la Arsenal

No comments

Powered by Blogger.