LIONEL MESSI ATUPIA MBILI BARCELONA IKIICHAKAZA SEVILLA

  Lionel Messi amefunga magoli mawili wakati Barcelona ikiibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Sevilla na kuendelea kuitia tumbo joto Real Madrid katika kuwania ubingwa wa La Liga. Katika mchezo huo wageni Barcelona waliutawala mpira huo tangu mwanzo na walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Luis Suarez aliyefunga kwa tik-taka. Messi alifunga goli la pili kufuatia pande la Suarez alilolipiga kwa kuurudisha mpira nyuma na kisha akaongeza la tatu kwa shuti kali.
                                         Luis Suarez akifunga goli la kwanza kwa kupiga tik-taka
                            Neymar akikata mbunga kupeleka mashambulizi kwenye lango la Sevilla

No comments

Powered by Blogger.