Kingu Awaahidi Wanasingida Kama Watachagua Diwani Wa CCM Basi Atabeba Majukumu Yote Ya Tundu Lissu
Mbunge
wa Singida Magharibi Elibariki Kingu amewaahidi wananchi wa Kata ya
Siuyu jimbo la Singida Mashariki kuwa endapo watamchagua mgombea udiwani
wa CCM, atakuwa mlezi wao na kwenda kuwasemea bungeni kuhusu matatizo
ya maji waliyonayo, jukumu ambalo linapaswa kufanywa na Lissu ambaye
ndiye mbunge wa hapo.
Mh.
Kingu ametoa ahadi hiyo wakati akimnadi mgombea wa Udiwani kata ya
Siuyu Wilayani Ikungi Mkoani Singida ambapo mbali na kuahidi kuwa mlezi
wa kata hiyo amewaahidi wakina mama kuwapatia Milioni 15 katika mfuko wa
VICOBA endapo watafanikisha kumpatia ushindi mgombea huyo wa CCM Mgonto
Juma Ramadhani
"Mimi
kama Mbunge wa Singida Magharibi naahidi na nitayatekeleza baada ya
uchaguzi wa tarehe 26. Nitatoa milioni 15 kwa ajili ya kata ya Siuyu
peke yake na Ofisi za chama mmesema kwamba hamna viti nitawapatia
Milioni moja kwa ajili ya viti. Nimepewa taarifa kuna vijiji havina maji
hii agenda ya Siuyu nitaibeba na nitaipeleka Dodoma kuiwasilisha na
baada ya hapo nitamleta Waziri wa Maji kuja kutatua hiyo changamoto",
amesema Kingu
'Nimeogopa
kuja na hizo fedha hapa kwa sababu watasema nahonga hivyo nitasubiri
mpaka uchaguzi upite ndiyo nilete ili nisije kuchafua hali ya hewa kwa
sasa" Kingu.
Kwa
upande wa Mgombea wa Kata hiyo amewaomba wananchi kumchagua ili aende
kuwawakilisha katika baraza la madiwani katika kutatua tatizo la maji
ambalo lipo kwa mda mrefu na tatizo la barabara ambayo ni mbovu.
Uchaguzi
katika kata ya Siuyu unafanyika baada ya Diwani Gerald Mahami
aliyekuwepo kutoka (CHADEMA) kuvuliwa udiwani kutokana na kuwepo madai
ya kushindwa kuhudhuria vikao vya baraza la madiwani.
Post a Comment