Uongozi Yanga wafikia maamuzi juu ya ‘Donald Ngoma’

                                                                  Donald Ngoma 
 Uongozi wa Klabu ya Yanga SC umefikia maamuzi ya kukaa chini na mshambuliaji wao, Donald Ngoma na kujadili vitendo vyake vya utovu wa nidhamu ndani ya timu hiyo.
Ngoma mwenye misimu miwili Jangwani, amekumbwa na kashfa za kuondoka na kugomea kuichezea timu hiyo kwa kisingizio cha kuwa majeruhi msimu huu na kuwa na msaada kidogo ndani ya timu hiyo kutokana na kutocheza mara kwa mara kwa sababu ya majeraha ya goti ambalo limemfanya akose michezo mingi ya timu hiyo.
Uongozi wa Yanga SC kupitia kwa Katibu wa Klabu hiyo, Boniface Mkwasa amesema wataongea kwa kina na mshambuliaji huyo juu ya safari yake ya Afrika Kusini alipokwenda kutibiwa na kuzidisha siku.
Tunatarajia kuwa na kikao na Ngoma kutokana na mwenendo wake kwa msimu huu ambapo amekuwa akikaidi baadhi ya vitu ambavyo tunakubaliana ikiwemo juu ya safari yake ya Afrika Kusini aliyoenda hivi karibuni, Tulimpa ruhusa ya kwenda kutibiwa huko ili akamalize tatizo lake la goti ambalo linamsumbua lakini yeye alipitisha siku ambazo tulimpa na kuendelea kukaa huko bila ya idhini yetu na bila ya kuuambia uongozi lolote lile“Alisema Boniface Mkwasa na kutoa Onyo
Sasa tunataka tumbane kwa ajili ya kujua nini kilichotokea maana ilisemekana kuwa alifanya mazungumzo na baadhi ya timu hivyo tunataka kujua kama ni kweli au la ili tuweze kumchukulia hatua za kinidhamu,” alisema Mkwasa kwenye mahojiano yake na Gazeti la Championi.
Licha mchezaji huyo kuuchanganya Uongozi wa Simba bado Kocha mkuu wa Klabu hiyo George Lwandamina anamhitaji kwa ajili ya kuimarisha safu ya mashambulizi .
a utovu wa nidhamu ndani ya timu hiyo.

No comments

Powered by Blogger.