Waziri wa Kikwete Afikishwa Kortini
NAIBU waziri wa fedha wa awamu
ya nne kwenye uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Adam Kighoma Ali
Malima leo Mei 16, 2017 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu akituhumiwa kuwazuia polisi kufanya kazi yao.
Mlalamikaji katika kesi hiyo ni askari
H.7818 PC Abdul akiwa kazini na maafisa wa Kampuni ya PBEL
inayojihusisha na kukamata watu wanaopaki magari hovyo ambapo tukio hilo
lilitokea jana eneo la Double Tree Hotel Masaki.
Mlalamikaji amedai alizuiliwa
kutekeleza wajibu wake na waziri mstaafu huyo huku akishirikiana na
wananchi kuwazuia askari hao ambapo askari huyo aliamua kupiga risasi
sita hewani ili kuwatuliza watu waliokuwa wanazomea wakiongozwa na
mtuhumiwa.Hata hivyo mtuhumiwa pamoja na dereva wake walikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi Oysterbay jana na kufunguliwa kesi yenye namba OB/RB/7306/2017.
Aidha mahakama imemwachilia huru Malima kwa dhamana ya shilingi milioni tano.
Post a Comment