EDEN HAZARD ATUPIA MBILI NA KUIPA USHINDI CHELSEA

 Chelsea inaongoza kwa tofauti ya pointi saba kileleni dhidi ya Tottenham baada ya kupambana mno kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Manchester City.

Kwa kipigo hicho kikosi cha Pep Guardiola kimekubali kipigo cha nyumbani na ugenini kutoka kwa Chelsea kwa mara ya kwanza chini ya kocha huyo.

Katika mchezo huo Eden Hazard aliipatia Chelsea goli la kuongoza katika dakika ya 10 baada ya shuti alilopiga kumgonga Vincent Kompany na kumpita kipa Willy Caballero.

Kipa wa Chelsea Thibaut Courtois alifanya kosa katika kuokoa na kutoa mwanya kwa David Silva kumtengenezea nafasi ya kufunga Sergio Aguero.

Fernandinho alimchezea rafu Pedro na kutolewa penati ambayo licha ya kipa Cabellero kuiokoa penati iliyopigwa na Hazard, mpira ulimrudia na akatumbukiza la pili.
  Kipa wa Manchester City Willy Caballero akichanganyikiwa baada ya kufungwa
        Sergio Aguero akishangilia baada ya kufunga goli pekee la Man City

No comments

Powered by Blogger.