Aunty Ezekiel : Siwezi tena 'ku-kiss' Kwenye Movie
Star
wa Bongo Movie nchini mwanadada Aunty Ezekiel, amerudi upya kwenye
tasnia hiyo huku akiweka wazi baadhi ya mabadiliko aliyoyafanya katika
maisha yake kuwa ni pamoja na kutoweza tena 'ku-kiss' kwenye movie
atakazocheza.
Aunty
ambaye kwa sasa amerejea na movie mpya inayokwenda kwa jina la
Chritmass Eve, amesema kilichomfanya afikie maamuzi hayo ni majukumu
aliyonayo kwa sasa ya kifamilia ikiwa ni pamoja na malezi ya mtoto.
Akiwa
kwenye kipindi cha FNL cha EATV Aunty amesema kuanzia sasa akiwa kwenye
movie, kabla hajakubali ku-kiss na mtu kwanza anamkumbuka mtoto wake
huku akitaja mabadiliko mengine kuwa ni kuweza kuigiza kama 'house girl'
uhusika ambao awali aliwahi kusema hawezi kuuigiza.
"Nimechenji
baada ya kuzaa, nimekuwa na mawazo tofauti, nimerudi nyuma mara mbili
hata ikitokea kwenye movie natakiwa ku-kiss, najifikiria sana hivi
mwanangu akiona atafikiria nini" Alisema
Amesema
hivi sasa amebadilika kwa kuwa amekuwa mtu mzima na kusisitiza kuwa kwa
sasa ameacha mabo yote ya kitoto aliyokuwa akiyafanya ikiwemo kuishi
kwa skendo maana ameona hayana faida.
Katika hatua nyingine Aunt alisema anatarajia kupata mtoto wa pili ambaye angependa awe wa kike
Post a Comment