WADAU WAJADILI MPANGO KAZI WA KUENDESHA SHUGHULI ZA SERIKALI KWA UWAZI (OGP) WA AWAMU YA TATU

 Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan P. Mlawi akisisitiza jambo kuhusu Mpango Kazi wa Kuendesha Shughuli za Serikali kwa Uwazi ( OGP) wa Awamu ya Tatu wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili mpango huo, uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TWAWEZA Bw. Aidan Eyakuze akichangia mada katika mkutano wa wadau wa kujadili Mpango Kazi wa Kuendesha Shughuli za Serikali kwa Uwazi (OGP) wa Awamu ya Tatu, uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wadau waliohudhuria mkutano wa kujadili Mpango Kazi wa Kuendesha Shughuli za Serikali kwa Uwazi ( OGP) wa Awamu ya Tatu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ikulu Bw. Peter Ilomo (hayupo pichani) wakati akiwasilisha hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Ikulu Bw. Peter Ilomo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa kujadili Mpango Kazi wa Kuendesha Shughuli za Serikali kwa Uwazi ( OGP) wa Awamu ya Tatu uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es salaam. Bw. Ilomo alifungua mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb)

No comments

Powered by Blogger.